HABARI MPYA
blink
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Development stories. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Development stories. Onyesha machapisho yote

JE UNATAFUTA KAZI? HII NI NJIA BORA YA KUPATA AJIRA

Written By Unknown on Jumanne, 17 Novemba 2015 | 02:51



Je, umejaribu #RecruitMe unapotafuta ajira Tanzania?

Ukosefu wa ajira ni changamoto kubwa duniani kote. Hili linasikitisha kwa kuwa kazi ni chanzo cha heshima binafsi, amani na utulivu.Tanzania, miongoni mwa nchi za dunia ya tatu, imechukua hatua muhimu katika kuendeleza sekta yake ya ajira, japo bado inakabiliwa na changamoto kubwa katika hilo. Asilimia kubwa ya watanzania wenye uwezo wa kufanya kazi, aidha hawana ajira au ajira walizonazo haziendani na uwezo wao.

Kutokana na ushindani mkubwa katika soko la ajira na ongezeko kubwa la vijana wanaoingia kwenye soko la ajira (800,000 hadi 1,000,000 kwa mwaka), sekta rasmi imekosa mafanikio katika kuzalisha fursa za ajira, hasa mijini.  Matokeo yake ni; kiwango cha umasikini kimeongezeka.

Sababu kuu zinazochangia fursa duni za ajira ni pamoja na:
·         Kutokuwa na usawa kati ya supply ya wafanyakazi na mahitaji. Ukweli ni kwamba, supply ya wafanyakazi ni kubwa kuliko demand ya wafanyakazi katika soko la ajira. Kila mwaka tunashuhudia ongezeko la vijana wanaomaliza masomo yao ambao wanaingia mtaani kuongeza idadi ya watafutao kazi.
·         Vijana kukimbilia kutafuta kazi mijini. Asilimia kubwa ya vijana wakimaliza elimu yao, hufikiria kwenda mijini kutafuta ajira, na wengi wao huwa na mawazo ya kufanya kazi ‘za ofisini’. Hili linasababisha shinikizo na ushindani mkubwa wa fursa za ajira. Laiti kama vijana wengi wangeamua kujikita katika sekta ya kilimo cha kisasa au sekta nyingine tofauti tofauti kwa kutumia elimu yao, ongezeko la watafutao kazi mjini lingepungua kwa kiasi kikubwa.
·         Elimu duni. Hili linajumuisha kutokujua kusoma na kuandika na ukosefu wa mafunzo sahihi yanayomuandaa mtu kuingia katika soko la ajira. Hakuna mwajiri anayeweza kuajiri mtu asiye na stadi muhimu za kitaaluma zinazohitajika katika kazi. Inaaminika kuwa, zaidi ya 61% ya wahitimu wanakuwa hawako tayari kiushindani katika soko la ajira.
Kutokana na mwangaza huo wa hali halisi ya ajira nchini Tanzania mradi wa #RecruitMe umejipanga kusaidia kila mwenye uwezo wa kufanya kazi, vijana na wazee ili waweze kupata ajira wanazotaka. Tunafahamu kwamba ukosefu wa kazi ni jambo linalotatiza wengi na wengi kuhisi kuwa wamenyimwa haki yao kama binadamu ndani ya jamii wanayoishi.

Kwa hiyo, #RecruitMe kwa makusudi mazima imeamua kujitolea kuweka jukwaa ambalo kila mtu anaweza kulitumia anapotafuta ajira sahihi na kupitia jukwaa hilo, mtu anaweza kugundua fursa mpya zilizopo katika soko la ajira. Zaidi ya hayo, waajiri wanaweza kunufaika sana kutokana na jukwaa hili, kwa kuwa linatoa fursa kwao pia kutafuta wafanyakazi wanaowahitaji.

Lengo kuu la mradi huu si kuwapa watu ajira yeyote tu, la hasha, bali ni kuwapatia watu ajira zenye hadhi, heshima na kufanya ndoto za mtu kuwa kweli. #RecruitMe itakupatia ajira inayokubalika kisheria, yenye mapato yanayoendana na kiwango cha kazi na ujuzi wako. Tunakuthibitishia ajira itakayojali haki zako kama mwanadamu na mfanyakazi, ikiwa ni pamoja na kujali maslahi yako.

Ili kupata huduma zetu, tafadhali tembelea tovuti yetu http://goo.gl/zPLquy ambapo utakuwa na uwezo wa kuona fursa za ajira mbalimbali, pamoja na kujenga profile yako mwenyewe. Huna haja tena ya kutokwa na jasho kutembea kutoka ofisi moja hadi nyingine tu na kuishia kunyimwa nafasi. Pumzika, na tembelea tovuti yetu. Tunaweza kukusaidia kupata kazi uitakayo.

MFUMO DUME WAKWAZA WANAWAKE TANZANIA

Written By Unknown on Alhamisi, 2 Oktoba 2014 | 09:07



Imeelezwa kuwa mfumo dume ni moja ya changamoto zinazokwamisha wananwake nchini Tanzania katika harakati za kushiriki uongozi wa kijamii na uchumi.

Hayo yamebainishwa na afisa kutoka shirika la umoja wa mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO, Bi. Rose Mwalimu katika mahojiano maalumu.

Bi. Rose amebainisha kuwa wanawake wananyimwa fursa kutokana na mfumo dume jambo ambalo linatia shaka kama usawa wa hamsini kwa hamsini utapatikana ifikapo 2015 katika uwakilishi wa vyombo vya maamuzi.

Aidha Bi. Rose amebainisha kuwa licha ya jamii kutegemea vyombo vya habari katika kubadili tabia kwa njia ya habari, bado waandishi wa habari Tanzania havijatoa mchango wake kuondoa mfumo dume na unyanyasaji wa kijinsia

Akielezea juu ya weledi wa waandishi wa habari Tanzania Bi Rose mwalimu ambaye pia kitaaluma ni veteran katika taaluma ya habari, amewatahadharisha waandishi wa habari kuwa makini na waepuke kuandika habari zenye kuchochea migogoro.

Shirika la UNESCO linaendesha mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka katika Radio jamii nchini ili kuwajengea uwezo wa kuandika habari na kuandaa vipindi kwa kuzingatia masuala ya jinsi na jinsia.

Zaidi ya Radio Jamii 11 zimepata udhamini wa mafunzo na kujengewa uwezo na UNESCO ambayo yamefanyika kati ya September 22 na October mosi ambayo yamefanyika mkoani Kigoma pamoja na Mwanza.

WAHANGA WA MVUA 2013 WATELEKEZWA KIGOMA

Written By Unknown on Jumapili, 14 Septemba 2014 | 09:42

Na. Emanuel Senny, Kigoma. 
Bi. Bahati Luseba akiwa na wanawe katika eneo ilipokuwa nyumba yake


WAHANGA 100 wa mafuliko yaliyotokea mwaka 2013 maeneo ya katosho, kata ya Kibirizi katika manispaa ya Kigoma Ujiji wameachwa bila msaada wowote huku wakiishi maisha ya kutangatanga sambamba na kutotakiwa kujenga upya kutokana na eneo hilo kutengwa ili kupisha ujenzi wa bandari ya nchi kavu. 

Akifafanua hilo Mjane Bahati Luseba alisema yeye ni miongoni mwa wahanga ambapo alipoteza nyumba yake na anaoishi kwa kutangatanga kutafuta mahali pa kuishi hali inayowalazimu watoto wake watano wakiwemo wawili wa kike walale katika nyumba isiyosalama huku akisubiri fedha za fidia ambazo hajui atapewa lini. 

 Alisema aliishi hapo zaidi ya miaka 40 ndipo Desemba ,2013 walipokutwa na mafuriko, ambayo yalibomoa nyumba yake na kumlazimu alale nje zaidi ya miezi kumi akisubiri hatma ya malipo ya fidia kutoka serikalini ili aondokane na adha ya kutangatanga . 

Baada ya nyumba yangu kuharibika, mganga wa zahanati ya jibulenu alinipa chumba kwa muda katika zahanati yake , na kwasasa nimesaidiwa na mwalimu Gombea baada ya kutoka kutoka katika Zahanati kwani ni mahari pa wagonjwa tu alisema Luseba. 
Mabaki ya nyumba ziliezuliwa na Kimbunga wakati mvua kali
 Aliongeza kuwa taarifa zilizotoka Halmashauri kuwa kuna nyumba alitaftiwa kwaajiri ya makazi sio kweli pia mahema ambayo inasemekana walipewa baadhi ya wahanga hakuziona kwahiyo taarifa sio za kweli kwani yeye bado anatangatanga. 

Dkt. wa Zahanati ya Jibulenu Abu Rashid alikiri kumhifadhi katika chumba kimoja katika zahanati kutokana na mvua zilizokuwa zikiendelea. 

Nilishindwa kuendelea kumhuhifadhi kutokana na sheria,kanuni na taratibu za kikazi kuwa, zahanati si makazi rasmi kwa asiye mgonjwa aliongeza Rashidi. 

Aidha Kagu Jumanne ambaye ni mmoja wa wahanga wa mafuriko alisema kuwa baada ya tukio viongozi walienda eneo husika na kuahidi kutoa msaada kwa waathirika wote ila mpaka sasa hakuna walichopewa na wanaendelea kuhifadhiwa kwa majirani. 

Akijibia malamiko hayo Diwani wa kata husika Rashid Yunus ambaye pia ni Kaimu Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji alisema changamoto ya kushindwa kuwasaidia wahanga wa mafuriko inatokana na idadai kubwa ya walengwa na walitoa tulubai 52 kwa kaya 9 sambamba na kuyafungia mabati ili kuepusha lawama kwa umma kutokana na hali duni za wahanga hao. 

Hata hivyo Yunus alisema kuwa manispaa, ilitoa mabati chakavu 70, ili wapewe wananchi wenye maisha duni , lakini kutokana na ukubwa wa familia hizo wameamua kuyafungia katika ofisi ya serikali ya mtaa wa kahabwa katosho wakisubiri mchakato wa kufidiwa kwa wahanga hao ambao eneo lao limeteuliwa kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa Bandari kavu.

MAONESHO YA BIASHARA SIDO KIGOMA 2014 YAFANA

Written By Unknown on Jumanne, 2 Septemba 2014 | 03:41

Bw. McDonald Maganga, Meneja wa SIDO Kigoma

Maonesho ya bidhaa zinazozalishwa na viwanda vidogovidogo kanda ya kati yamemalizika kwa mafanikio makubwa mjini Kigoma nchini Tanzania huku yakiacha changamoto kadhaa za mitaji na masoko ya bidhaa husika.

Washiriki wa maonesho hayo kutoka mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora na mwenyeji Kigoma wamekiri kuwepo kwa matatizo ya mitaji pamoja na ukosefu wa soko la uhakika ndani na nje ya nchi, jambo linalodhoofisha wamiliki wa viwanda na wajasiriamali.
Sehemu ya Mabanda yaliyotumika katika maonesho ya biashara maarufu kama maonesho ya SIDO Kigoma
Wakiongea na mtandao huu katika kilele cha maonesho hayo  wameomba serikali na taaisisi zake kuwawezesha wajasiliamali kupata mitaji kwa njia ya mikopo yenye riba nafuu pamoja fursa za masoko.

Mmoja wa washiriki wa maonesho hayo Bi. Cotrida Kokupima kutoka wilayani Kasulu Mkoani Kigoma, amesema licha ya serikali kuwa na sera nzuri za kusaidia wajasiriamali bado taasisi za fedha hasa Benki hazijatoa unafuu kwao.
Naye Bw.Hamis Rudonongo kutoka Dodoma amesema watumishi wa umma katika kada ya chini, wanakiuka maadili ya utumishi wao kwa kuwanyima huduma wajasiriamali wadogo.
Kwa upande wake meneja wa shirika la maendeleo ya viwanda vidogo SIDO mkoani Kigoma Bw. McDonald Magnaga ambaye ndiye alikuwa mwenyeji wa maonesho hayo amesema licha ya changamoto zinazotajwa na wadau, maonesho hayo ya mwaka yamekuwa ufunguo wa fursa za masoko

Licha ya kukiri kuwepo kwa tatizo la soko la nje ya Tanzania, McDonald amebainisha kuwa SIDO inao mfuko maalumu kwa kuwakopesha Mitaji wajasiriamali wanaotimiza vigezo.
Bw. McDonald Maganga amebainisha kuwa Shirika hilo la viwanda vidogo linazo fursa za mikopo ambapo waasiriamali hukopeshwa kati ya sh. milioni mbili hadi sita. 

Zaidi ya wajasiriamali 270 kutoka mikoa ya kanda ya kati pamoja na nchini Kenya wameshiriki maonesho hayo.

Kwa mujibu wa taarifa za SIDO kiasi cha zaidi ya shilingi milioni mia mbili kimekopeshwa kwa wajasiriamali wadogowadogo katika kipindi cha mwaka 2013/2014



MAONESHO YA WANASAYANSI CHIPUKIZI (YOUNG SCIENTISTS) TANZANIA YAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

Written By Unknown on Alhamisi, 21 Agosti 2014 | 09:22


Sanamu ya Ndege iliyoungwa na mmoja wa wanasayansi chipukizi wa Tanzania

Na. Mwandishi wetu 
Dar es Salaam

Maonesho pamoja na sherehe ya kuwatunukia zawadi washindi wa wanasayansi chipukizi au Young Scientists Tanzania (YST) yalifanyika  tarehe 13 hadi 14 mwezi Agosti katika ukumbi wa Aghakhan Diamond Jublee. 


Maonesho haya walifadhiliwa na British Gas Tanzania pamoja na Irish Aid kwa matarajio kuwa vijana hawa wakiendelezwa tatizo la afrika kukosa wana sanyansi litakwisha


Mgeni rasmi wa maonesho hayo alikua Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Mohammed Gharib Bilal akifuatana na  Balozi wa Ireland nchini Tanzania Finneoula Gilsenan pamoja na Waziri Prof. Makame M. Mbarawa ambao pia walihudhuria maonesho hayo
Makamu wa Rais Dr. Gharib Bilal akisalimiana na meneja wa kampuni ya British Gas Bw. Adam Prince wakati wa Maonyesho hayo

Wanafunzi 200 na walimu kutoka mikoa mbalimbali Tanzania walikusanyika jijini Dar es Salaam kuonyesha miradi yao ya utafiti mwaka huu. 

Ongezeko la msaada unaotolewa na  BG(British Gas) Tanzania na Ireland Aid (Shirika la msaada la Ireland),kumewezesha  maonyesho ya wanasayansi chipukizi   kuwafikia wanafunzi  vijana kwa wingi zaidi ndani ya mwaka huu  2014.

Maonyesho ya( YST ) 2014 ni muendelezo wa mafanikio yaliyofikiwa miaka ya nyuma kutoka shule 4 mwaka 2011 hadi kufikia shule  100 mwaka huu.

Robn Damas na Michael Laurent wanafunzi kutoka Ilboru sekondari wakifurahia tuzo
Programu ya YST ilitokana na jitihada za Ireland ambayo ilitumia mfumo wa maendeleo ya elimu kupitia (CDPC) Combat Diseases of Poverty Consortium. (Kundi  la kupambana na maradhi yanayotokana na umaskini.

Wanafunzi watakaoshinda watawezesha shule zao kukua kisayansi na maendeleo. Zawadi zilizomo ni laptops, fedha, scholarships, pamoja na vitabu kwa maktaba za shule. Washindi wa jumla  wa YST 2014 wataalikwa kuhudhuria maonyesho ya BT Young Scientists na Teknolojia yatakayofanyika nchini Ireland mnamo Januari 2015. 

Kila mwaka maonyesho YST yanalenga  kuongeza mafanikio katika jitihada za  kuinua kiwango cha elimu ya sayansi katika shule za sekondari Tanzania . 

Maonyesho  yanaelezea   miradi kutoka makundi mbalimbali ya sayansi, kibaiolojia na ikolojia; fizikia na kemia; masomo ya kijamii na kitabia; na teknolojia.

Young Scientists Tanzania inatoa wito kwa shule zote nchini kujipatia fursa ya kukua kisayansi na kubadilisha mfumo wa kujifunza masomo ya Sayansi kwa kupitia mashindano hayo. Mashinda hayo hufanyika kila mwaka jijini Dar es Salaam na huhusisha zaidi ya shule 100.
 
Shukrani kwa : Harold Dickson | Prosper Kwigize | 0752490120
Copyright © 2013. KWIGIZE NEWS AND COMMUNICATION - Haki zote zimeifadhiwa
Email us: kwigizenews@gmail.com
0764243377